Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Muhammad   Ayah:
وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَوۡلَا نُزِّلَتۡ سُورَةٞۖ فَإِذَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ مُّحۡكَمَةٞ وَذُكِرَ فِيهَا ٱلۡقِتَالُ رَأَيۡتَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ نَظَرَ ٱلۡمَغۡشِيِّ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡمَوۡتِۖ فَأَوۡلَىٰ لَهُمۡ
Na wale wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanasema, «Basi si iteremshwe sura kutoka kwa Mwenyezi Mungu ituamrishe kupigana jihadi na wakanushaji.» Na inapoteremshwa sura iliyoimarika kwa maelezo na mambo ya lazima na ikatajwa jihadi ndani yake, utawaona wale ambao mna shaka ndani ya nyoyo zao juu ya Dini ya Mwenyezi Mungu na unafiki wanakuangalia, ewe Nabii, maangalizi ya mtu ambaye amefinikwa na kicho cha kufa.
Arabic explanations of the Qur’an:
طَاعَةٞ وَقَوۡلٞ مَّعۡرُوفٞۚ فَإِذَا عَزَمَ ٱلۡأَمۡرُ فَلَوۡ صَدَقُواْ ٱللَّهَ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡ
Basi lililo bora kwa hawa ambao ndani ya nyoyo zao mna maradhi wamtii Mwenyezi Mungu na wasema neno linaoafikiana na Sheria. Vita vinapopasa na ikaja amri ya Mwenyezi Mungu kuilazimisha, hawa wanafiki wanachukia hilo. Na lau wao wangalikuwa wakweli kwa Mwenyezi Mungu katika kuamini na kutenda mema, hilo lingalikuwa bora kwao kuliko kufanya maasia na kuenda kinyume.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَهَلۡ عَسَيۡتُمۡ إِن تَوَلَّيۡتُمۡ أَن تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَتُقَطِّعُوٓاْ أَرۡحَامَكُمۡ
Huenda nyinyi mkikipa mgongo Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Mwenendo wa Nabii wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, mkaja kumuasi Mwenyezi Mungu katika ardhi, mkamkanusha Yeye, mkamwaga damu na mkakata vizazi vyenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُ فَأَصَمَّهُمۡ وَأَعۡمَىٰٓ أَبۡصَٰرَهُمۡ
Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Amewaepusha na rehema Yake Akawafanya wasiyasikie yanayowanufaisha wala wasiyaone na zisiwafunukie hoja za Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa ni nyingi.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ ٱلۡقُرۡءَانَ أَمۡ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقۡفَالُهَآ
Je, si wayazingatie mawaidha ya Qur’ani wanafiki hawa na wazifikirie hoja zake? Lakini nyoyo hizi zimefungwa, hakuna kitu cha hii Qur’ani kinachozifikia, hivyo basi haziyatii akilini mawaidha ya Mwenyezi Mungu na mazingatio yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱرۡتَدُّواْ عَلَىٰٓ أَدۡبَٰرِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡهُدَى ٱلشَّيۡطَٰنُ سَوَّلَ لَهُمۡ وَأَمۡلَىٰ لَهُمۡ
Hakika ya wale waliyorudi nyuma wakaacha uongofu na Imani na wakageuka kwa visigino vyao wakimkanusha Mwenyezi Mungu baada ya haki kuwafunukia, (hao) Shetani amewapambia makosa yao na akawanyoshea matumaini ya kuishi duniani.
Arabic explanations of the Qur’an:
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُواْ لِلَّذِينَ كَرِهُواْ مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ سَنُطِيعُكُمۡ فِي بَعۡضِ ٱلۡأَمۡرِۖ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ إِسۡرَارَهُمۡ
Kule kuwanyoshea wao mpaka wakolee kwenye ukafiri, ni kwa kuwa wao walisema kuwaambia Mayahudi waliokanusha Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, «Tutawatii katika baadhi ya mambo ambayo yako kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na amri ya Mtume Wake.» Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anayajua wanayoyaficha na wanayoydhihirisha. Basi Muislamu ajihadhari na kumtii asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika mambo yaliyo kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, na amri ya Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَكَيۡفَ إِذَا تَوَفَّتۡهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يَضۡرِبُونَ وُجُوهَهُمۡ وَأَدۡبَٰرَهُمۡ
Basi itakuwa vipi hali yao watakapozikamata Malaika roho zao na huku wanawapiga nyuso zao na migongo yao?
Arabic explanations of the Qur’an:
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱتَّبَعُواْ مَآ أَسۡخَطَ ٱللَّهَ وَكَرِهُواْ رِضۡوَٰنَهُۥ فَأَحۡبَطَ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Adhabu hiyo waliyostahili na wakaipata ni kwa kuwa wao waliyafuata mambo yanayomfanya Mwenyezi Mungu Awakasirikie ya kumtii Shetani na wakayachukia yale yanayomfanya Awe radhi nao ya matendo mema, na miongoni mwayo ni kupigana na wakanushaji, baada ya kulifanya hilo ni lazima juu yao, ndipo Mwenyezi Mungu Akazibatilisha thawabu za matendo yao, miongoni mwa sadaka, kuunga kizazi na yasiyokuwa hayo.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَمۡ حَسِبَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَن لَّن يُخۡرِجَ ٱللَّهُ أَضۡغَٰنَهُمۡ
Au kwani wanadhani hao wanafiki kuwa Mwenyezi Mungu Hatovitoa vile vilivyomo ndani ya nyoyo zao vya uhasidi na kuuchukia Uislamu na wafuasi wake? Ndio, Mwenyezi Mungu Atamtenganisha mkweli kutokana na mrongo.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Muhammad
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis - Translations’ Index

Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Sh. Naser Khamis

close