Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Ash-Shūra   Ayah:
وَمِنۡ ءَايَٰتِهِ ٱلۡجَوَارِ فِي ٱلۡبَحۡرِ كَٱلۡأَعۡلَٰمِ
Na miongoni mwa alama Zake zenye kuonyesha uweza Wake mkubwa na mamlaka Yake yenye kushinda ni majahazi makubwa kama majabali yanayotembea baharini.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِن يَشَأۡ يُسۡكِنِ ٱلرِّيحَ فَيَظۡلَلۡنَ رَوَاكِدَ عَلَىٰ ظَهۡرِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّكُلِّ صَبَّارٖ شَكُورٍ
Anapotaka Mwenyezi Mungu Anautuliza upepo, na majahazi yakawa ni yenye kutulia juu ya mgongo wa bahari na kutotembea. Hakika katika kutembea majahazi haya na kusimama kwake baharini kwa uweza wa Mwenyezi Mungu pana mawaidha na hoja waziwazi za uweza wa Mwenyezi Mungu, kwa kila mwingi wa uvumilivu juu ya kumtii Mwenyezi Mungu, kujiepusha na vitendo vya kumuasi na kukubali makadirio Yake, mwingi wa shukrani wa neema Zake na mema Yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَوۡ يُوبِقۡهُنَّ بِمَا كَسَبُواْ وَيَعۡفُ عَن كَثِيرٖ
Au (Anapotaka) Anayaangamiza hayo majahazi kwa kuyazamisha kwa sababu ya dhambi za wenyewe, na Anasamehe dhambi nyingi Asiwatese wenye kuzifanya.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِنَا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٖ
Na wajue wale wanaojadili kuhusu aya zetu zenye kutolea dalili upweke wetu kwa njia ya ubatilifu, hawatakuwa na mahali pa kupita wala pa kuhamia kujiepusha na mateso ya Mwenyezi Mungu Atakapowatesa kwa dhambi zao na ukanushaji wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَمَآ أُوتِيتُم مِّن شَيۡءٖ فَمَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ
Na chochote kile mnachopewa, enyi watu, cha mali na watoto na vinginevyo, ni pumbao lenu la uhai wa ulimwenguni, kwa haraka sana litaondoka, na kilichoko kwa Mwenyezi Mungu cha starehe ya Pepo ya daima ni bora zaidi na ni chenye kusalia zaidi kwa wale wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake na wakawa kwa Mola wao wanategemea.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ وَإِذَا مَا غَضِبُواْ هُمۡ يَغۡفِرُونَ
Na wale ambao wanajiepusha na madhambi makubwa yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu, na kila kilichokuwa kichafu na kibaya miongoni mwa maasia, na wanapowakasirikia wale waliowakosea wanaufinika huo ubaya na kuusamehe kwa kuacha kumlipiza mkosa, kwa kutaka malipo mema ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na msamaha Wake. Na hii ni miongoni mwa tabia njema.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّذِينَ ٱسۡتَجَابُواْ لِرَبِّهِمۡ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَمۡرُهُمۡ شُورَىٰ بَيۡنَهُمۡ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ
Na wale walioitika mwito wa Mola wao wa kumpwekesha Yeye na kumtii, wakasimamisha Swala za faradhi kwa namna zake katika nyakati zake, na wakitaka jambo wanashauriana juu yake , na katika mali tuliyowapa wanatoa sadaka kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, na wanatekeleza haki wanazofaradhiwa kuwapatia wanaostahiki kama vile Zaka na matumizi na katika njia nyinginezo za matumizi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَابَهُمُ ٱلۡبَغۡيُ هُمۡ يَنتَصِرُونَ
Na wale ambao yakiwapata maonevu wanawalipiza wale waliowaonea bila kupita kiasi. Na wanaposubiri basi mwisho wa subira yao kuna kheri nyingi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَجَزَٰٓؤُاْ سَيِّئَةٖ سَيِّئَةٞ مِّثۡلُهَاۖ فَمَنۡ عَفَا وَأَصۡلَحَ فَأَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلظَّٰلِمِينَ
Na malipo ya ubaya wa mtu mbaya ni kumtesa kwa ubaya mfano wake bila kuzidisha. Na mwenye kumsamehe aliyemfanyia ubaya asimtese, na akatengeneza mapenzi baina yake yeye na yule aliyemsamehe kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, basi malipo mema ya kusamehe kwake yako kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi wenye kudhulumu wanaowaanza watu kwa uadui na kuwafanyia ubaya.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَمَنِ ٱنتَصَرَ بَعۡدَ ظُلۡمِهِۦ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَا عَلَيۡهِم مِّن سَبِيلٍ
Na yoyote aliyemlipiza yule aliyemdhulumu baada ya kudhulumiwa naye, basi hao hawana makosa ya kuadhibiwa kwayo.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّمَا ٱلسَّبِيلُ عَلَى ٱلَّذِينَ يَظۡلِمُونَ ٱلنَّاسَ وَيَبۡغُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Hakika ni kwamba mapatilizo ni ya wale wanaowaonea watu kwa udhalimu na uadui, wakapita mpaka waliowekewa wa vitu walivyohalalishiwa na Mola wao na wakaingia kwenye eneo la vitu visivyoruhusiwa kwao, wakafanya uharibifu katika ardhi pasi na haki, basi hao Siku ya Kiyama watakuwa na adhabu yenye uchungu na kuumiza.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنۡ عَزۡمِ ٱلۡأُمُورِ
Na yoyote mwenye kuvumilia juu ya makero na akalipa, kwa ovu alilofanyiwa, kwa kusamehe, kufuta na kufinika, basi hayo ni miongoni mwa mambo makubwa yenye kushukuriwa na vitendo vyenye kusifiwa ambavyo Mwenyezi Mungu Ameviamrisha na Ameviwekea thawabu nyingi na sifa nzuri.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِن وَلِيّٖ مِّنۢ بَعۡدِهِۦۗ وَتَرَى ٱلظَّٰلِمِينَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَ يَقُولُونَ هَلۡ إِلَىٰ مَرَدّٖ مِّن سَبِيلٖ
Na yule ambaye Mwenyezi Mungu Anampoteza na kumweka kando na uongofu kwa sababu ya udhalimu wake, hatakuwa na mtu wa kumsaidia na kumuelekeza njia ya uongofu. Na utawaona, ewe Mtume, wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, watakapo kuiona adhabu, wakisema, kumwambia Mola wao, «Je, tuna njia yoyote ya kurejea duniani ili tufanye matendo ya utiifu kwako?» Na ombi hilo halitakubaliwa kwao.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Ash-Shūra
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis - Translations’ Index

Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Sh. Naser Khamis

close