Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Tā-ha   Ayah:

Taha

طه
«Ṭā, Hā» Yametangulia maelezo kuhusu herufi za mkato mwanzo wa sura ya Al -Bqarah.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ لِتَشۡقَىٰٓ
Hatukuiteremsha Qur’ani kwako, ewe Mtume, ujisumbue kwa jambo usiloliweza kulifanya.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَّا تَذۡكِرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰ
Lakini tumeiteremsha iwe ni mawaidha, ili ajikumbushe nayo mwenye kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu apate kujikinga nayo kwa kutekelaza faradhi na kujiepusha na mambo ya haramu.
Arabic explanations of the Qur’an:
تَنزِيلٗا مِّمَّنۡ خَلَقَ ٱلۡأَرۡضَ وَٱلسَّمَٰوَٰتِ ٱلۡعُلَى
Hii Qur’ani ni teremsho kutoka kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Ameumba ardhi na mbingu zilizo juu.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلرَّحۡمَٰنُ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ ٱسۡتَوَىٰ
Mwingi wa rehema, juu ya 'Arsh Amelingana, yaani Amekuwa juu na Ameangatika, kulingana kunakonasibiana na utukufu Wake na ukubwa Wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَمَا تَحۡتَ ٱلثَّرَىٰ
Ni Vyake vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini na vilivyoko baina yake na vilivyoko ndani yake, kwa kuviumba, kuvitamalaki na kuviendesha.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِن تَجۡهَرۡ بِٱلۡقَوۡلِ فَإِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلسِّرَّ وَأَخۡفَى
Na ukitoa sauti, ewe Mtume, katika kusema ukaifanya ya juu au ya chini, basi hakuna chochote kinachofichika kwa Mwenyezi Mungu, Anajua siri na kilichofichika zaidi kuliko siri katika vitu ambavyo nafsi yako inakuzungumzia.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ لَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ
Mwenyezi Mungu Ambaye hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, ni Yake Peke Yake majina yaliyokamilika katika uzuri.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَهَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
Na je, imekujia, ewe Mtume, habari ya Mūsā bin ‘Imrān, amani imshukie, katika kurudi kwake kutoka Madyan na kuelekea Misri.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِذۡ رَءَا نَارٗا فَقَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّيٓ ءَانَسۡتُ نَارٗا لَّعَلِّيٓ ءَاتِيكُم مِّنۡهَا بِقَبَسٍ أَوۡ أَجِدُ عَلَى ٱلنَّارِ هُدٗى
Alipouona moto usiko umewashwa, akasema kuwaambia watu wa nyumbani kwake, «Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikawaletea kinga cha moto mkapata kujitoa ubaridi na mkawasha moto mwingine kwa kinga hiko, au nikapata mtu wa kutuongoza njia.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَمَّآ أَتَىٰهَا نُودِيَ يَٰمُوسَىٰٓ
Mūsā alipoufikia ule moto, Mwenyezi Mungu Alimuita, «Ewe Mūsā!
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنِّيٓ أَنَا۠ رَبُّكَ فَٱخۡلَعۡ نَعۡلَيۡكَ إِنَّكَ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوٗى
Mimi ni Mola wako, vua viatu vyako, wewe sasa uko kwenye bonde la Tuwā nililolipa baraka. Hivyo ni ili ajiandae kusema na Mola wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Tā-ha
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis - Translations’ Index

Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Sh. Naser Khamis

close