Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: An-Nahl   Ayah:
وَتَحۡمِلُ أَثۡقَالَكُمۡ إِلَىٰ بَلَدٖ لَّمۡ تَكُونُواْ بَٰلِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ ٱلۡأَنفُسِۚ إِنَّ رَبَّكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ
Na wanabeba wanyama hawa vyombo vyenu vizito kuvipeleka kwenye mji wa mbali ambao hamkuwa ni wenye kuufikia isipokuwa kwa usumbufu mwingi wa nafsi zenu na mashaka makubwa. Hakika Mola wenu ni Mpole, Mwenye huruma kwenu kwa kuwafanyia vitu mnavyovitaka kuwa vipesi. Hivyo basi kusifiwa ni Kwake na kushukuriwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلۡخَيۡلَ وَٱلۡبِغَالَ وَٱلۡحَمِيرَ لِتَرۡكَبُوهَا وَزِينَةٗۚ وَيَخۡلُقُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Na Amewaumbia farasi, nyumbu na punda, mpate kuwapanda na wawe ni pambo kenu nyinyi na maangalizi mazuri. Na Anawaumbia nyinyi aina mbalimbali za vipando na vinginevyo ambavyo nyinyi hamna ujuzi navyo, ili mzidi kumuamini na kumshukuru.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَعَلَى ٱللَّهِ قَصۡدُ ٱلسَّبِيلِ وَمِنۡهَا جَآئِرٞۚ وَلَوۡ شَآءَ لَهَدَىٰكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuwaeleza njia iliolingana sawa ya kuwaongoa nyinyi, nayo ni Uislamu. Na miongoni mwa njia kuna iliyoenda kombo isiyofikisha kwenye uongofu, nayo ni kila njia iliyo kinyume na Uislamu miongoni mwa mila na itikadi. Na lau Angalitaka Mwenyezi Mungu kuwaongoza, basi Angaliwaongoza nyote kwenye Imani.
Arabic explanations of the Qur’an:
هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗۖ لَّكُم مِّنۡهُ شَرَابٞ وَمِنۡهُ شَجَرٞ فِيهِ تُسِيمُونَ
Yeye Ndiye Aliyewateremshia mvua kutoka juu na Akawapatia nyinyi kwa hiyo mvua maji mnayokunywa na akawatolea kwa maji hayo miti ya nyinyi kuwalisha wanyama wenu, na yanarudi kwenu matumizi yake na manufaa yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
يُنۢبِتُ لَكُم بِهِ ٱلزَّرۡعَ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلنَّخِيلَ وَٱلۡأَعۡنَٰبَ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ
Anawatolea nyinyi kutoka kwenye ardhi, kwa maji haya mamoja, mazao mbalimbali: Anawatolea nyinyi kwayo mizaituni, mitende na mizabibu, na anawatolea nyinyi kwayo kila aina ya matunda, makubwa kwa madogo. Hakika katika hayo pana ushahidi waziwazi kwa watu wanaofikiri na wakazingatia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ وَٱلنُّجُومُ مُسَخَّرَٰتُۢ بِأَمۡرِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ
Na Amewadhalilishia usiku kwa mapumziko yenu, na mchana kwa maisha yenu, na Amewadhalilishia jua likawa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na ili mpate kujua miaka na hesabu na manufaa mengine yasiyokuwa hayo. Na nyota huko mbinguni zimedhalilishwa kwa ajili yenu kwa amri ya Mwenyezi Mungu, ili mjue nyakati, kuiva kwa matunda na mazao na pia kuongoka kwa nyota hizo kwenye giza. Hakika, katika kudhalilisha huko, kuna alama waziwazi kwa watu wanaotia mambo akilini mwao kuhusu Mwenyezi Mungu, hoja Zake na alama Zake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا ذَرَأَ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُخۡتَلِفًا أَلۡوَٰنُهُۥٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَذَّكَّرُونَ
Na Amewadhalilishia vile Alivyowaumbia katika ardhi miongoni mwa vinavyotambaa humo na matunda na madini na visivyokuwa hivyo ambavyo vina rangi na manufaa mbalimbali. Hakika katika uumbaji huo na kutafautiana rangi na manufaa pana mazingatio kwa watu wanaowaidhika na wanaojua kwamba katika kuvidhalilisha vitu hivyi pana alama nyingi juu ya umoja wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na juu ya kumpwekesha kwa ibada.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَهُوَ ٱلَّذِي سَخَّرَ ٱلۡبَحۡرَ لِتَأۡكُلُواْ مِنۡهُ لَحۡمٗا طَرِيّٗا وَتَسۡتَخۡرِجُواْ مِنۡهُ حِلۡيَةٗ تَلۡبَسُونَهَاۖ وَتَرَى ٱلۡفُلۡكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Na Yeye Ndiye Ambaye Amewadhalilishia bahari ili mpate kula nyama laini ya samaki mnaowavua, na mtoe humo pambo mnalolivaa kama lulu na marjani, na utaziona jahazi kubwa zinapasua uso wa maji zikienda na kurudi, na mnazipanda ili mtafute riziki ya Mwenyezi Mungu kwa kufanya biashara na kutafuta faida ndani yake. Kwani huenda nyinyi mkamshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa neema zake kubwa juu yenu na msimuabudu asiyekuwa Yeye.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: An-Nahl
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis - Translations’ Index

Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Sh. Naser Khamis

close