Check out the new design

Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Cibiyar fassara ta Ruwwad * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Fassarar Ma'anoni Sura: Al'ma'arij   Aya:
يُبَصَّرُونَهُمۡۚ يَوَدُّ ٱلۡمُجۡرِمُ لَوۡ يَفۡتَدِي مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِئِذِۭ بِبَنِيهِ
Ijapokuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe.
Tafsiran larabci:
وَصَٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ
Na mkewe, na nduguye.
Tafsiran larabci:
وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِي تُـٔۡوِيهِ
Na jamaa zake waliokuwa wakimkimu,
Tafsiran larabci:
وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا ثُمَّ يُنجِيهِ
Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye.
Tafsiran larabci:
كَلَّآۖ إِنَّهَا لَظَىٰ
La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa,
Tafsiran larabci:
نَزَّاعَةٗ لِّلشَّوَىٰ
Unaobambua ngozi ya kichwa!
Tafsiran larabci:
تَدۡعُواْ مَنۡ أَدۡبَرَ وَتَوَلَّىٰ
Utamwita kila aliyegeuza mgongo na akageuka.
Tafsiran larabci:
وَجَمَعَ فَأَوۡعَىٰٓ
Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi.
Tafsiran larabci:
۞ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا
Hakika mtu ameumbwa na papara.
Tafsiran larabci:
إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعٗا
Inapomgusa shari hupapatika.
Tafsiran larabci:
وَإِذَا مَسَّهُ ٱلۡخَيۡرُ مَنُوعًا
Na inapomgusa kheri huizuilia.
Tafsiran larabci:
إِلَّا ٱلۡمُصَلِّينَ
Isipokuwa wanaosali.
Tafsiran larabci:
ٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ دَآئِمُونَ
Ambao wanadumisha Sala zao.
Tafsiran larabci:
وَٱلَّذِينَ فِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ مَّعۡلُومٞ
Na ambao katika mali yao iko haki maalumu.
Tafsiran larabci:
لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ
Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba;
Tafsiran larabci:
وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo.
Tafsiran larabci:
وَٱلَّذِينَ هُم مِّنۡ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشۡفِقُونَ
Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.
Tafsiran larabci:
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمۡ غَيۡرُ مَأۡمُونٖ
Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo.
Tafsiran larabci:
وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ
Na ambao wanahifadhi tupu zao.
Tafsiran larabci:
إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ
Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi.
Tafsiran larabci:
فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ
Lakini wanaotaka kinyume cha haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka.
Tafsiran larabci:
وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَٰنَٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٰعُونَ
Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,
Tafsiran larabci:
وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَٰدَٰتِهِمۡ قَآئِمُونَ
Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,
Tafsiran larabci:
وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ
Na ambao wanazihifadhi Sala zao.
Tafsiran larabci:
أُوْلَٰٓئِكَ فِي جَنَّٰتٖ مُّكۡرَمُونَ
Hao ndio watakaoheshimiwa katika Bustani ya mbinguni.
Tafsiran larabci:
فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ قِبَلَكَ مُهۡطِعِينَ
Wana nini wale waliokufuru wanakutumbulia macho tu?
Tafsiran larabci:
عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ
Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!
Tafsiran larabci:
أَيَطۡمَعُ كُلُّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ أَن يُدۡخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٖ
Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Bustani ya mbinguni ya neema?
Tafsiran larabci:
كَلَّآۖ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّمَّا يَعۡلَمُونَ
La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanachokijua.
Tafsiran larabci:
فَلَآ أُقۡسِمُ بِرَبِّ ٱلۡمَشَٰرِقِ وَٱلۡمَغَٰرِبِ إِنَّا لَقَٰدِرُونَ
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza.
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Sura: Al'ma'arij
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Cibiyar fassara ta Ruwwad - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

Wani gungu na cibiyar fassara ta Ruwad ne suka fassarasu tare da haɗin gwiwar Ƙungiyar Da'awa ta Rabwah da Kungiyar hidimtawa abinda Musulunci ya kunsa da yaruka

Rufewa