Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center * - Translations’ Index

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Translation of the meanings Surah: Al-Muddaththir   Ayah:
فَقُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ
Basi ameangamia! Vipi alivyopima!
Arabic explanations of the Qur’an:
ثُمَّ قُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ
Tena ameangamia! Vipi alivyopima!
Arabic explanations of the Qur’an:
ثُمَّ نَظَرَ
Kisha akatazama.
Arabic explanations of the Qur’an:
ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ
Kisha akakunja kipaji, na akanuna.
Arabic explanations of the Qur’an:
ثُمَّ أَدۡبَرَ وَٱسۡتَكۡبَرَ
Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَقَالَ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ يُؤۡثَرُ
Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا قَوۡلُ ٱلۡبَشَرِ
Haya si chochote ila kauli ya binadamu.
Arabic explanations of the Qur’an:
سَأُصۡلِيهِ سَقَرَ
Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سَقَرُ
Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?
Arabic explanations of the Qur’an:
لَا تُبۡقِي وَلَا تَذَرُ
Haubakishi wala hausazi.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَوَّاحَةٞ لِّلۡبَشَرِ
Unababua ngozi iwe nyeusi.
Arabic explanations of the Qur’an:
عَلَيۡهَا تِسۡعَةَ عَشَرَ
Juu yake wapo kumi na tisa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا جَعَلۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَٰٓئِكَةٗۖ وَمَا جَعَلۡنَا عِدَّتَهُمۡ إِلَّا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيَسۡتَيۡقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَيَزۡدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِيمَٰنٗا وَلَا يَرۡتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ وَٱلۡكَٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَمَا يَعۡلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡبَشَرِ
Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha waliokufuru, wapate kuwa na yakini waliopewa Kitabu, na wazidi Imani wale walioamini, wala wasiwe na shaka waliopewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndiyo kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anayejua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binadamu.
Arabic explanations of the Qur’an:
كَلَّا وَٱلۡقَمَرِ
Hasha! Naapa kwa mwezi!
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّيۡلِ إِذۡ أَدۡبَرَ
Na kwa usiku unapokucha!
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلصُّبۡحِ إِذَآ أَسۡفَرَ
Na kwa asubuhi inapopambazuka!
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّهَا لَإِحۡدَى ٱلۡكُبَرِ
Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!
Arabic explanations of the Qur’an:
نَذِيرٗا لِّلۡبَشَرِ
Ni onyo kwa binaadamu.
Arabic explanations of the Qur’an:
لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَتَقَدَّمَ أَوۡ يَتَأَخَّرَ
Kwa anayetaka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa.
Arabic explanations of the Qur’an:
كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡ رَهِينَةٌ
Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyoyachuma.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡيَمِينِ
Isipokuwa watu wa kuliani.
Arabic explanations of the Qur’an:
فِي جَنَّٰتٖ يَتَسَآءَلُونَ
Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana
Arabic explanations of the Qur’an:
عَنِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Habari za wakosefu:
Arabic explanations of the Qur’an:
مَا سَلَكَكُمۡ فِي سَقَرَ
Ni nini kilichokupelekeni Motoni?
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ لَمۡ نَكُ مِنَ ٱلۡمُصَلِّينَ
Waseme: Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَمۡ نَكُ نُطۡعِمُ ٱلۡمِسۡكِينَ
Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ ٱلۡخَآئِضِينَ
Na tulikuwa tukizama pamoja na waliozama katika maovu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na tulikuwa tukiikanusha Siku ya Malipo.
Arabic explanations of the Qur’an:
حَتَّىٰٓ أَتَىٰنَا ٱلۡيَقِينُ
Mpaka yakini ilipotufikia.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Al-Muddaththir
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center - Translations’ Index

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

close