Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center * - Translations’ Index

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Translation of the meanings Surah: Ibrāhīm   Ayah:

Ibrahim

الٓرۚ كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ إِلَيۡكَ لِتُخۡرِجَ ٱلنَّاسَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذۡنِ رَبِّهِمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ
Alif Laam Raa.[1] Hiki ni Kitabu tulichokuteremshia ili uwatoe watu kwenye giza mbalimbali uwapeleke kwenye mwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifika.
[1] Herufi hizi "Alif Laam Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱللَّهِ ٱلَّذِي لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَوَيۡلٞ لِّلۡكَٰفِرِينَ مِنۡ عَذَابٖ شَدِيدٍ
Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye vyote vilivyo katika mbingu zote na katika ardhi. Na ole wao makafiri kwa adhabu kali!
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلَّذِينَ يَسۡتَحِبُّونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا عَلَى ٱلۡأٓخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبۡغُونَهَا عِوَجًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ فِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدٖ
Wale wanaofadhilisha uhai wa dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wako katika upotofu wa mbali.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوۡمِهِۦ لِيُبَيِّنَ لَهُمۡۖ فَيُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Na hatukumtuma Mtume yeyote isipokuwa kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Mwenyezi Mungu anampoteza amtakaye, na anamwongoa amtakaye. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ أَنۡ أَخۡرِجۡ قَوۡمَكَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ وَذَكِّرۡهُم بِأَيَّىٰمِ ٱللَّهِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّكُلِّ صَبَّارٖ شَكُورٖ
Na hakika tulimtuma Musa na miujiza yetu, tukamwambia: Watoe kaumu yako kwenye giza mbalimbali uwapeleke kwenye nuru. Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kila mwenye kusubiri sawasawa, mwenye kushukuru sana.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ أَنجَىٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ وَيُذَبِّحُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ
Na Musa alipowaambia kaumu yake, "Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu pale alipowaokoa kutokana na watu wa Firauni waliokuwa wakiwatia adhabu mbaya kabisa, wakiwachinja wana wenu wanaume, na wakiwaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo ulikuwa mtihani mkubwa unaotoka kwa Mola wenu Mlezi."
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذۡ تَأَذَّنَ رَبُّكُمۡ لَئِن شَكَرۡتُمۡ لَأَزِيدَنَّكُمۡۖ وَلَئِن كَفَرۡتُمۡ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٞ
Na alipotangaza Mola wenu Mlezi: Mkishukuru, hakika nitawazidishia. Na mkikufuru, basi adhabu yangu ni kali.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَالَ مُوسَىٰٓ إِن تَكۡفُرُوٓاْ أَنتُمۡ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا فَإِنَّ ٱللَّهَ لَغَنِيٌّ حَمِيدٌ
Na Musa alisema: Mkikufuru nyinyi na wote walio katika dunia, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifika.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَبَؤُاْ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ قَوۡمِ نُوحٖ وَعَادٖ وَثَمُودَ وَٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ لَا يَعۡلَمُهُمۡ إِلَّا ٱللَّهُۚ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَرَدُّوٓاْ أَيۡدِيَهُمۡ فِيٓ أَفۡوَٰهِهِمۡ وَقَالُوٓاْ إِنَّا كَفَرۡنَا بِمَآ أُرۡسِلۡتُم بِهِۦ وَإِنَّا لَفِي شَكّٖ مِّمَّا تَدۡعُونَنَآ إِلَيۡهِ مُرِيبٖ
Je, hazikuwafikia habari za wale waliokuwa kabla yenu? Kaumu ya Nuhu, na 'Aadi, na Thamud, na wale waliokuwa baada yao, ambao hakuna awajuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu? Mitume wao waliwajia na hoja zilizo wazi, na wao wakarudisha mikono yao kwenye vinywa vyao, wakasema: Hakika sisi tumeyakufuru hayo mliyotumwa nayo, na hakika sisi tuko katika shaka kubwa na hayo mnayotuitia.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ قَالَتۡ رُسُلُهُمۡ أَفِي ٱللَّهِ شَكّٞ فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يَدۡعُوكُمۡ لِيَغۡفِرَ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمۡ وَيُؤَخِّرَكُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗىۚ قَالُوٓاْ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُنَا تُرِيدُونَ أَن تَصُدُّونَا عَمَّا كَانَ يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَا فَأۡتُونَا بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ
Mitume wao wakasema: Ati kuna shaka kuhusiana na Mwenyezi Mungu, Muumba mbingu na ardhi? Yeye anawaita ili awafutie madhambi yenu, na awape muhula mpaka muda uliowekwa. Wakasema: Nyinyi si chochote isipokuwa ni wanadamu tu kama sisi. Mnataka kutuzuilia mbali na yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu. Basi tujieni na hoja iliyo wazi.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَتۡ لَهُمۡ رُسُلُهُمۡ إِن نَّحۡنُ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَمَا كَانَ لَنَآ أَن نَّأۡتِيَكُم بِسُلۡطَٰنٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ
Mitume wao wakawaambia: Sisi kweli si chochote isipokuwa ni wanadamu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humneemesha amtakaye katika waja wake. Wala sisi hatuwezi kuwaletea uthibitisho isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu basi na wategemee Waumini.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا لَنَآ أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى ٱللَّهِ وَقَدۡ هَدَىٰنَا سُبُلَنَاۚ وَلَنَصۡبِرَنَّ عَلَىٰ مَآ ءَاذَيۡتُمُونَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ
Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ametuongoa kwenye njia zetu. Na hakuna hakika tutayavumilia hayo maudhi mnayotuudhi nayo. Na juu ya Mwenyezi Mungu na wategemee wanaotegemea.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِرُسُلِهِمۡ لَنُخۡرِجَنَّكُم مِّنۡ أَرۡضِنَآ أَوۡ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَاۖ فَأَوۡحَىٰٓ إِلَيۡهِمۡ رَبُّهُمۡ لَنُهۡلِكَنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ
Na wale waliokufuru wakawaambia Mitume wao: Hakika, tutawatoa katika nchi yetu, au lazima mtarudi katika mila yetu. Basi Mola wao Mlezi akawafunulia ufunuo (wahyi): Hakika tutawaangamiza madhalimu!
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَنُسۡكِنَنَّكُمُ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡۚ ذَٰلِكَ لِمَنۡ خَافَ مَقَامِي وَخَافَ وَعِيدِ
Na hakika tutawaweka kukaa katika ardhi baada yao. Haya ni kwa anayehofu kusimamishwa mbele yangu, na akahofu ahadi yangu ya adhabu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱسۡتَفۡتَحُواْ وَخَابَ كُلُّ جَبَّارٍ عَنِيدٖ
Na wakaomba ushindi, na akashindwa kila jabari mkaidi.
Arabic explanations of the Qur’an:
مِّن وَرَآئِهِۦ جَهَنَّمُ وَيُسۡقَىٰ مِن مَّآءٖ صَدِيدٖ
Nyuma yake iko Jahannamu, na atanyweshwa katika maji ya usaha.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَتَجَرَّعُهُۥ وَلَا يَكَادُ يُسِيغُهُۥ وَيَأۡتِيهِ ٱلۡمَوۡتُ مِن كُلِّ مَكَانٖ وَمَا هُوَ بِمَيِّتٖۖ وَمِن وَرَآئِهِۦ عَذَابٌ غَلِيظٞ
Awe anayagugumiza, wala hataweza kuyameza. Na mauti yatamjia kutokea kila upande, wala hatakufa. Na zaidi ya hayo itakuwepo adhabu nyengine kali.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَّثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡۖ أَعۡمَٰلُهُمۡ كَرَمَادٍ ٱشۡتَدَّتۡ بِهِ ٱلرِّيحُ فِي يَوۡمٍ عَاصِفٖۖ لَّا يَقۡدِرُونَ مِمَّا كَسَبُواْ عَلَىٰ شَيۡءٖۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلضَّلَٰلُ ٱلۡبَعِيدُ
Mfano wa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi, vitendo vyao ni kama jivu linalopeperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya upepo mkali. Hawawezi kupata chochote katika yale waliyoyachuma. Huko ndiko kupotea kwa mbali!
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ وَيَأۡتِ بِخَلۡقٖ جَدِيدٖ
Je, huoni kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki? Akitaka, anawaondoa na alete viumbe wapya!
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ بِعَزِيزٖ
Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si jambo gumu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَبَرَزُواْ لِلَّهِ جَمِيعٗا فَقَالَ ٱلضُّعَفَٰٓؤُاْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُوٓاْ إِنَّا كُنَّا لَكُمۡ تَبَعٗا فَهَلۡ أَنتُم مُّغۡنُونَ عَنَّا مِنۡ عَذَابِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۚ قَالُواْ لَوۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ لَهَدَيۡنَٰكُمۡۖ سَوَآءٌ عَلَيۡنَآ أَجَزِعۡنَآ أَمۡ صَبَرۡنَا مَا لَنَا مِن مَّحِيصٖ
Na wote watajitokeza mbele ya Mwenyezi Mungu. Wanyonge watawaambia wale waliotakabari: Hakika sisi tulikuwa wafwasi wenu; basi hebu mtuondolee kidogo hivi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Lau Mwenyezi Mungu angelituongoa, basi hakuna shaka nasi tungeliwaongoa. Ni mamoja kwetu tukipapatika au tukisubiri; hatuna popote pa kukimbilia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَالَ ٱلشَّيۡطَٰنُ لَمَّا قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ إِنَّ ٱللَّهَ وَعَدَكُمۡ وَعۡدَ ٱلۡحَقِّ وَوَعَدتُّكُمۡ فَأَخۡلَفۡتُكُمۡۖ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيۡكُم مِّن سُلۡطَٰنٍ إِلَّآ أَن دَعَوۡتُكُمۡ فَٱسۡتَجَبۡتُمۡ لِيۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوٓاْ أَنفُسَكُمۖ مَّآ أَنَا۠ بِمُصۡرِخِكُمۡ وَمَآ أَنتُم بِمُصۡرِخِيَّ إِنِّي كَفَرۡتُ بِمَآ أَشۡرَكۡتُمُونِ مِن قَبۡلُۗ إِنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Na shetani atasema itakapokatwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi ahadi ya kweli. Nami niliwaahidi; lakini sikuwatimizia ahadi yangu. Na sikuwa na mamlaka yoyote juu yenu, isipokuwa niliwaita, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamuwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikufuru tangu zamani huko kunishirikisha kwenu na Mwenyezi Mungu. Hakika madhalimu wana adhabu chungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأُدۡخِلَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا بِإِذۡنِ رَبِّهِمۡۖ تَحِيَّتُهُمۡ فِيهَا سَلَٰمٌ
Na wale walioamini na wakatenda mema wataingizwa katika Mabustani yapitayo mito kwa chini yake, wadumu humo kwa idhini ya Mola wao Mlezi. Maamkizi yao humo yatakuwa: Salaam (Amani)!
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا كَلِمَةٗ طَيِّبَةٗ كَشَجَرَةٖ طَيِّبَةٍ أَصۡلُهَا ثَابِتٞ وَفَرۡعُهَا فِي ٱلسَّمَآءِ
Je, hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyopiga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni.
Arabic explanations of the Qur’an:
تُؤۡتِيٓ أُكُلَهَا كُلَّ حِينِۭ بِإِذۡنِ رَبِّهَاۗ وَيَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ
Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٖ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ ٱجۡتُثَّتۡ مِن فَوۡقِ ٱلۡأَرۡضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٖ
Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, uliong'olewa juu ya ardhi. Hauna uimara wowote.
Arabic explanations of the Qur’an:
يُثَبِّتُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱلۡقَوۡلِ ٱلثَّابِتِ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۖ وَيُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلظَّٰلِمِينَۚ وَيَفۡعَلُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ
Mwenyezi Mungu huwaimarisha wale walioamini kwa kauli ya imara katika uhai wa dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwapoteza madhalimu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ بَدَّلُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ كُفۡرٗا وَأَحَلُّواْ قَوۡمَهُمۡ دَارَ ٱلۡبَوَارِ
Je, hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na wakawafikisha kaumu yao kwenye nyumba ya maangamizo?
Arabic explanations of the Qur’an:
جَهَنَّمَ يَصۡلَوۡنَهَاۖ وَبِئۡسَ ٱلۡقَرَارُ
Nayo ni Jahannamu wataiingia! Na ni mahali pa kukaa pabaya mno!
Arabic explanations of the Qur’an:
وَجَعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادٗا لِّيُضِلُّواْ عَن سَبِيلِهِۦۗ قُلۡ تَمَتَّعُواْ فَإِنَّ مَصِيرَكُمۡ إِلَى ٱلنَّارِ
Na walimfanyia Mwenyezi Mungu wenza ili wapoteze watu kutoka kwenye njia yake. Sema: Stareheni! Kwani maishio yenu ni Motoni!
Arabic explanations of the Qur’an:
قُل لِّعِبَادِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُنفِقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ يَوۡمٞ لَّا بَيۡعٞ فِيهِ وَلَا خِلَٰلٌ
Waambie waja wangu walioamini, wadumishe Swala, na watoe katika tulivyowaruzuku, kwa siri na dhahiri, kabla ya kufika kwa Siku isiyokuwa na biashara yoyote wala urafiki wa dhati.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزۡقٗا لَّكُمۡۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلۡفُلۡكَ لِتَجۡرِيَ فِي ٱلۡبَحۡرِ بِأَمۡرِهِۦۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلۡأَنۡهَٰرَ
Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akawatiishia majahazi yanayokwenda baharini kwa amri yake, na akawatiishia mito.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ دَآئِبَيۡنِۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ
Na akawatiishia jua na mwezi vinavyokwenda daima dawamu, na akawatiishia usiku na mchana.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَءَاتَىٰكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلۡتُمُوهُۚ وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآۗ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَظَلُومٞ كَفَّارٞ
Na akawapa katika kila mlichomuomba. Na mkihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamuwezi kuzidhibiti. Hakika mwanadamu ni dhalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِيمُ رَبِّ ٱجۡعَلۡ هَٰذَا ٱلۡبَلَدَ ءَامِنٗا وَٱجۡنُبۡنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعۡبُدَ ٱلۡأَصۡنَامَ
Na Ibrahim aliposema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu uwe wa amani, na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu.
Arabic explanations of the Qur’an:
رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضۡلَلۡنَ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُۥ مِنِّيۖ وَمَنۡ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hayo yamewapoteza wengi wa watu. Basi aliyenifuata mimi, huyo hakika ni miongoni mwangu. Na aliyeniasi, hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
Arabic explanations of the Qur’an:
رَّبَّنَآ إِنِّيٓ أَسۡكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيۡرِ ذِي زَرۡعٍ عِندَ بَيۡتِكَ ٱلۡمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱجۡعَلۡ أَفۡـِٔدَةٗ مِّنَ ٱلنَّاسِ تَهۡوِيٓ إِلَيۡهِمۡ وَٱرۡزُقۡهُم مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَشۡكُرُونَ
Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria yangu katika bonde lisilokuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili wadumishe Swala. Basi zifanye nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku matunda, ili wapate kushukuru.
Arabic explanations of the Qur’an:
رَبَّنَآ إِنَّكَ تَعۡلَمُ مَا نُخۡفِي وَمَا نُعۡلِنُۗ وَمَا يَخۡفَىٰ عَلَى ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ
Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe unajua tunayoyaweka hadharani na tunayoyaficha. Na hakuna kitu kinachofichikana kwa Mwenyezi Mungu katika ardhi wala katika mbingu.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى ٱلۡكِبَرِ إِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَۚ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ
Alhamdulillahi (sifa njema ni za Mwenyezi Mungu) aliyenitunuku pamoja na uzee wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia sana maombi.
Arabic explanations of the Qur’an:
رَبِّ ٱجۡعَلۡنِي مُقِيمَ ٱلصَّلَوٰةِ وَمِن ذُرِّيَّتِيۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلۡ دُعَآءِ
Mola wangu Mlezi! Nifanye niwe mwenye kudumisha Swala, na katika dhuria yangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ikubali dua yangu.
Arabic explanations of the Qur’an:
رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لِي وَلِوَٰلِدَيَّ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ يَوۡمَ يَقُومُ ٱلۡحِسَابُ
Mola wetu Mlezi! Nisamehe mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku itakaposimama hesabu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ غَٰفِلًا عَمَّا يَعۡمَلُ ٱلظَّٰلِمُونَۚ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمۡ لِيَوۡمٖ تَشۡخَصُ فِيهِ ٱلۡأَبۡصَٰرُ
Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika mbali na wanayoyafanya madhalimu. Hakika Yeye anawaahirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao.
Arabic explanations of the Qur’an:
مُهۡطِعِينَ مُقۡنِعِي رُءُوسِهِمۡ لَا يَرۡتَدُّ إِلَيۡهِمۡ طَرۡفُهُمۡۖ وَأَفۡـِٔدَتُهُمۡ هَوَآءٞ
Watakuwa mbioni, vichwa juu, huku macho yao hayapepesi, na nyoyo zao zitakuwa tupu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَنذِرِ ٱلنَّاسَ يَوۡمَ يَأۡتِيهِمُ ٱلۡعَذَابُ فَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ رَبَّنَآ أَخِّرۡنَآ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖ نُّجِبۡ دَعۡوَتَكَ وَنَتَّبِعِ ٱلرُّسُلَۗ أَوَلَمۡ تَكُونُوٓاْ أَقۡسَمۡتُم مِّن قَبۡلُ مَا لَكُم مِّن زَوَالٖ
Na waonye watu siku itakapowajia adhabu, na wale waliodhulumu waseme, "Ewe Mola wetu Mlezi! Tuahirishe muda kidogo tuitikie wito wako na tuwafuate Mitume." Kwani nyinyi hamkuapa zamani kwamba kamwe hamuwezi kuondoka?
Arabic explanations of the Qur’an:
وَسَكَنتُمۡ فِي مَسَٰكِنِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَتَبَيَّنَ لَكُمۡ كَيۡفَ فَعَلۡنَا بِهِمۡ وَضَرَبۡنَا لَكُمُ ٱلۡأَمۡثَالَ
Na mkakaa katika maskani zile zile za wale waliozidhulumu nafsi zao. Na ikawabainikia jinsi tulivyowatendea. Nasi tukawapigia mifano mingi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَدۡ مَكَرُواْ مَكۡرَهُمۡ وَعِندَ ٱللَّهِ مَكۡرُهُمۡ وَإِن كَانَ مَكۡرُهُمۡ لِتَزُولَ مِنۡهُ ٱلۡجِبَالُ
Na hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao hivyo anavijua Mwenyezi Mungu. Na kwa yakini vitimbi vyao hivyo vilikuwa ni vya kuweza kuondosha milima.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ مُخۡلِفَ وَعۡدِهِۦ رُسُلَهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٖ
Basi kamwe usimdhanie Mwenyezi Mungu kuwa ni mwenye kuwavunjia ahadi yake Mitume wake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Mwenye kulipiza.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَوۡمَ تُبَدَّلُ ٱلۡأَرۡضُ غَيۡرَ ٱلۡأَرۡضِ وَٱلسَّمَٰوَٰتُۖ وَبَرَزُواْ لِلَّهِ ٱلۡوَٰحِدِ ٱلۡقَهَّارِ
Siku itakapogeuzwa ardhi iwe ardhi nyingine, na mbingu zote pia. Nao watajitokeza mbele ya Mwenyezi Mungu Mmoja, Mshindi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَتَرَى ٱلۡمُجۡرِمِينَ يَوۡمَئِذٖ مُّقَرَّنِينَ فِي ٱلۡأَصۡفَادِ
Na utaona wahalifu siku hiyo wamefungwa katika minyororo.
Arabic explanations of the Qur’an:
سَرَابِيلُهُم مِّن قَطِرَانٖ وَتَغۡشَىٰ وُجُوهَهُمُ ٱلنَّارُ
Nguo zao zitakuwa za lami, na Moto utazigubika nyuso zao.
Arabic explanations of the Qur’an:
لِيَجۡزِيَ ٱللَّهُ كُلَّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ
Ili Mwenyezi Mungu ailipe kila nafsi yale iliyoyachuma. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.
Arabic explanations of the Qur’an:
هَٰذَا بَلَٰغٞ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُواْ بِهِۦ وَلِيَعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا هُوَ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ وَلِيَذَّكَّرَ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ
Huu ni ufikishaji kwa watu, ili waonywe kwao, na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja, na wapate kukumbuka wenye akili.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Ibrāhīm
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center - Translations’ Index

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

close